Masharti

  1. Mwombaji awe Mtanzania na mkazi katika Jimbo Katoliki la Bukoba (Wilaya za Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba, Missenye na Nkenge.)
  2. Mwombaji awe yatima aliyefiwa na Baba au Mama au wote au awe anatoka katika familia yenye uhitaji na hana mtu wa kumlipia karo.
  3. Mwombaji anapaswa kuwa tayari anasoma au amesajiliwa katika Chuo kinachotambuliwa na mamlaka husika Tanzania. Kwa waombaji wa shule za msingi na sekondari, BUCADOS inaweza kuwachagulia shule ya kujiunga na kuwasaidia katika usajili.
  4. Mwombaji asiwe mnufaika wa msaada mwingine wa kimasomo au mkopo wa serikali.

Namna ya Kutuma Maombi

  1. Mwombaji atatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuiwasilisha kwa mkono kwa Katibu wa BUCADOS Jimboni Bukoba au kuituma kwa njia ya barua pepe (email): info@bucados.iliwawenauzima.co.tz
  2. Fomu ya maombi inaweza kupakuliwa HAPA au inaweza kupatika katika ofisi ya parokia ya mwombaji.
  3. Mwombaji ataarifiwa matokeo ya mamobi yake kupitia anwani aliyoiweka kwenye fomu ya maombi.








Lengo la Shirika

Kusaidia kusomesha yatima maskini na watoto wenye uhitaji jimboni Bukoba ili kuwaandaa kushiriki katika kutatua changamoto za kiuchumi.

Soma zaidi


Saidia

Tunakaribisha msaada wa kifedha kutoka kwa watu binafsi na mashirika, kupitia Bank Transfer, Credit Card na PayPal.


Soma zaidi


Jiunge Nasi

Unakaribishwa kujiunga na Marafiki wa BUCADOS ili usaidie kuchangia na kueneza lengo la BUCADOS ili kuwafikia wafadhili wengi zaidi.

Jiunge


Copyright © 2024 Bukoba Catholic Diocese - All Rights Reserved

Designed by Creative Mind