Kusaidia kusomesha watoto yatima na wenye uhitaji katika jimbo la Bukoba ili kuwatayarisha waweze kuchangia katika kutatua changamoto za kiuchumi zinazokabili familia zao na jamii yao na kushiriki katika utume wa Kanisa kwa ajili ya wokovu wa watu.
Malengo Mahususi
BUCADOS inalenga kuwawezesha watoto yatima na wahitaji jimboni Bukoba kupitia elimu kwa kuwalipia karo na mahitaji mengine ya kimasomo. Malengo mahususi ya shirika hili yatajumuisha yafuatayo:
- Kuomba na kuchangisha fedha kutoka kwa wafadhili binafsi na mashirika ili kusomesha watoto yatima na wahitaji jimboni Bukoba.
- Kuanzisha na kuendesha shughuli za kiuchumi ili kuongeza kwenye fedha zilizochangwa katika kusaidia elimu ya watoto yatima na wahitaji.
- Kutoa ushauri nasaha kwa yatima ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto za kisaikolojia zinazotokana na kufiwa na wazazi.
- Kuzisaidia familia za watoto yatima wanaosaidiwa na BUCADOS kuanzisha shughuli za kiuchumi zitakazowasaidia kujitegemea na kuwasaidia watoto wengine ambao hawasaidiwi na BUCADOS.